SIMANJIRO-MANYARA
Na Wilberd Kiwale
Mchimbaji mdogo wa Madini ya Tanzanite (MwanaApolo) wa Mji mdogo wa
Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,amekutwa amefariki Dunia pembeni ya
barabara kwenye machimbo ya Madini Hayo.
Kamanda wa polisi Mkoani Manyara Kamishna msaidizi Liberatus Sabas,amemtaja
marehemu kuwa nai Jimmy Chawe (25) mkazi wa kitongoji cha Songambele,katika Mji mdogo
wa Mirerani.
Kamanda Sabas amesema Chawe amekutwa amekufa siku ya jumatatu saa 12:30 asubuhi,kwenye barabara iliyopo kwenye machimbo ya Madini ya
Tanzanite eneo la Mpaka wa kitalu D na kitalu C Mji mdogo wa Mirerani.
Chanzo cha kifo cha mchimbaji huyo ambaye ana Asili ya Kijiji cha
Pomelini Mkoani Iringa hakijafahamika mara Moja,na alikutwa akiwa na jeraha
dogo kwenye mguu wa kushoto.
Kamanda Sabas alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye
hospitali ya mkoa wa Arusha (Mount Meru) Kwa ajili ya uchunguzi zaidi Kabla ya
kusafirishwa kupelekwa Mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment