Monday, March 26, 2012

BWILO AKAMILISHA ZIARA SIMANJIRO

NADONJUKIN  SIMANJIRO


Na Jackson Mollel

Ziara ya Siku nne ya Mkuu wa mkoa wa manyara Bwana Elaston John Bwilo wilayani Simanjiro mkoani Manyara imekamilika katika kijiji Cha Nadonjukin kwa yeye kupokea kero na malalamiko mbalimali ya wakazi wa kijiji hicho.

Katika kikao hicho kilichokuwa na idadi kubwa ya kina mama  wa jamii ya Kimaasai wakazi wa kijiji hicho ambapo baathi yao walifika ofisini kwa mkuu wa Mkoa mjini Babat walisema kuwa sambamba na mambo mengine yaliyo kero  katika kijiji hicho, kubwa ni Uwekezaji wa Kampuni ya Ranchi ya Ormoti Tukuta Conservation  waliopo katika eneo lao.

Wamama hao waliwasilisha kero zao kwa mkuu huyo kwa kusoma risala iliyojaa tuhuma kwa kampuni ya Ormoti Tukuta Conservation ya kuwa wamepewa eneo lililo katika kijiji chao bila ya ridhaa yao.

Mara baada ya Risala hiyo iliyosomwa na  bibi Naomi Mbatiany,  Mkuu wa Mkoa  bwana Bwilo amesema kuwa kuna haja ya Kuchunguza jambo hilo kwa kina katika kufuata taratibu za kisheria ili kuweza kulipatia Ufumbuzi mapema. 
 
Bwana Bwilo amesema kuwa si rahisi kwa yeye kutamka mara moja ya kuwa eneo ni la nani lakini ameahidi kutuma wataalam wa ardhi kutoka mkoa ili kuja kubaini mipaka jambo litakaloleta Suluhu katika mgogoro huo.

Katika Kikao Hicho  kilicho Hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikale kutoka Mkoa na Wilaya, Mbuge wa Simanjiro mheshimiwa Christopha ole Sendeka alimuomba mkuu wa Mkoa kushirikisha wazee na viongozi wa Zamani katika zoezi hilo la kubaini mipaka hiyo.

Ole Sendeka amesema kuwa taratibu na mipango ya utoaji wa Ranchi hiyo haukufuata taratibu zinazo Stahili huku akimwomba mkuu huyo kuunda Tume itakayo chunguza nyaraka mbalimbali za uhalali wa kuwepo kwake katika eneo hilo.
                    

1 comment:

  1. thanks ors for good and interesting work by markodaniel9@gmail.com

    ReplyDelete