Saturday, March 24, 2012

MIUNDO MBINU WILAYANI SIMANJIRO BADO NI KIKWAZO CHA MAENDELEO
                                     Hii ni sehemu ya daraja lililoharibiwa na mvua na kusababisha
                                     adha kwa wananchi na wasfiri ndani ya wilaya ya Simanjiro na
                                     wilaya ya Kiteto

TERRAT-SIMANJIRO 24/3/2012
Na Julius Laizer
Wananchi wa kijiji cha Terrat na maeneo mengine wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wameiomba serikali kuhakikisha kuwa inarekebisha miundo mbinu ya bara bara ili kuwarahisishia majukumu yao mengi hasa kipindi hiki cha mvua

Wameyasema hayo kutokana na daraja lililoharibika katika kijiji cha Komolo na kuwasababishia ugumu wa usafiri wa wananchi watokao mji wa Arusha kuelekea makao makuu ya Wilaya na wanaoelekea Wilayani Kiteto

Daraja hilo limehaibika kufuatia mvua zilizonyesha mwaka jana na kubomoa sehemu kubwa ya daraja hilo hali iliyosababisha magari na wananchi kushindwa kulitumia na badala yake wanapita kwa pembeni

Jamii imeomba serikali kuchukua hatua za haraka kukarabati daraja hilo kwa kiwango cha hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wananchi wa wanafunzi wanapata usafiri kwa muda na wakati unaostahili

Wakielezea adha ya daraja hilo wafanyabiashara na waendesha magari wamesema mvua inaponyesha korongo hilo kupitisha maji mengi ambapo huwafanya wasubiri mpaka maji yapungue ndipo wapite hivyo bidhaa wanazobeba hurabika na kufika vikiwa vimepungua ubora wake hasa zile za sokoni

No comments:

Post a Comment