LOON`DEREKES
SIMANJIRO
Mkuu wa mkoa
wa Manyara bwana Elaston John Bwilo
amezindua Mradi wa Maji katika kijijicha Londerkes kata ya Kitwai Wilayani
Simanjiro mkoani Manyara Uliogharimu jumla ya shilingi Milioni 59 laki tisa 9
na 42 elfu
Kijiji hicho
ambacho ni kati ya vijiji 52 vya wilaya ya Simanjiro ni miongoni mwa vijiji
vilivyo na tatizo la uhaba wa maji ambapo wakazi wake wanalazimika kuchota maji
katika chemchem iliyopo umbali mrefu kutoka kijijini hapo.
Habari
kutoka Loondrekes zinasema kuwa awali wakaza wa kijiji hicho walikuwa wanapaata
maji katika Chemchem iliyopo mlimani, ambapo wanawake na watoto wakazi wa
kijiji hicho wemekuwa wakipata tabu wakati wa kwenda kuteka maji kutokana na
muinuko mkali wa mlima huo.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara mkuu huyo ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya
Simanjiro kupitia Vikao vya madiwani kuangalia kwa zaidi kwa macho mawili suala
la mifugo kwani ndiyo uchumi pekee unaotengemewa kwa asilimia kubwa na wakazi
wa wilaya ya Simanjiro.
Bwana Bwilo
ameiomba Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Kupitia Idara ya Mifugo kujenge
Majosho ya kisasa kwaajili ya kuogesha mifugo pamoja na kupatiwa Chanjo na mahitaji mengine muhimu kwa kadri taaluma
ya mifugo inavyoelekeza.
By Jackson M Mollel (KIONGOZI)
No comments:
Post a Comment