Hanang-Manyara
Na Wilberd Kiwale
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani manyara Winfrida Ligubi,amewataka wakazi wa kata ya Balangdalalu kutoa ushirikiano wa ulinzi wa shule ya secondary ya Bweni ya Balangdalalu,dhidi ya matukio ya kuungua moto.
Kanali Mstaafu Ligubi ametoa agizo hilo,kutokana na matukio ya
kuzuka moto mara Kwa mara kwenye Shule hiyo,na kusababisha kufungwa kwa kipindi
cha mwezi Mmoja Kwa ajili ya kukarabatiwa.
Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo juzi kwenye kikao cha Bodi ya
Shule hiyo,alipoitembelea kuona Maendeleo ya ukarabati wa Bweni Moja na madarasa
mawili yaliyoungua moto kwa siku tofauti.
Matukio ya kuungua moto kwa mabweni yalitokea Januari 31 Mwaka Huu
na tukio la pili kuungua moto Kwa madarasa mawili yalitokea Februari 16
Mwaka Huu na Chanzo cha kuzuka moto huo kikiwa bado hakijabainika.
Mkuu wa Shule hiyo GodlivingTyaso amesema ukarabati wa mabweni na madarasa
mwili yaliyoungua unaendelea vizuri,ingawa hawakupata Msaada wowote zaidi ya
Mfuko wa maafa,na amesema wanafunzi wanatarajia kurudi shuleni mwezi huu wa tatu tarehe 18.
No comments:
Post a Comment