Na Julius Laizer
waraka kwa asasi wilayani Kiteto
KITETO
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara,Frank Uhahula amesema atazichukulia hatua kali asasi zisizo za kiserikali ambazo zimeacha kufanya kile walichosajiliwa nacho na kushiriki kuleta uchochezi wilayani humo.
Uhahula ameyasema hayo hivi karibuni mjini Kibaya na kudai kuwa asasi nyingi wilayani humo zimeshiriki kuleta maendeleo ndani ya jamii lakini nyingine zimejivika mwamvuli wa vyama vya kisiasa na kujiingiza kwa kificho kwenye shughuli za kisiasa.
Amesema kuwa asasi hizo badala ya kuendeleza masuala waliyosajiliwa nayo ya maendeleo ndani ya jamii hushirikiana na baadhi ya vyama vya kisiasa katika kufanya uchochezi kwa wananchi.
Bwana huhaula amezitaka asasi hizo kuchague moja, kati ya uanasiasa au uwana harakati wa maendeleo ya kijamii ili watambue kwmba wanashindana nao kama vyama vingine katika kutaka kukamata dola maana hawaeleweki kama ni asasi ama vyama vya kisiasa
Ameongeza kuwa asasi hizo zisimchonganishe Rais Jakaya Kikwete na wananchi wake kwani zinatakiwa kuleta maendeleo kwa wananchi badala ya kujiingiza kisirisiri kwenye mambo ya kisiasa na kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa wilayani humo.
Na Julius Laizer
Uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki
ARUMERU
Chama cha D emokrasia na Maendeleo Chandema kimelitaka jeshi la Polisi kuwa sehemu ya matumaini na haki kwa wana wanchi wa Arumeru Mashariki na sio kuwatisha na kuwatio hofu.
Hayo yamesemwa na mwenyekitu wa chama cha Demokrasia na Maendelo Chadema mheshimiwa Freman Mbowe katika mikutano aliyoifanya katika jimbo la Arumeru Mashariki, katika vijiji vya Maruango Uwilo,Ushiri,Ambureni na Embaseni ya kumnadi mgombea ubunge wake bwana Joshua Nasari.
Nae manager wa Kampeni wa Chadema Mheshimiwa Vecent Nyerere akizungumza katika mikutano hiyo ameeleza kusikitishwa na kauli ya Chama cha Mapinduzi ya kuwataka wanachama wake kutohudhuria mikutano ya Chadema akisema kuwa ni kuwanyima haki yao ya msingi huku akiwataka wanachama wa Chadema na wapenda maendele kuhudhuria Mikutano ya ccm kusikiliza sera zao.
Kwa upande wake chama cha Mapinduzi kimeitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuchukua hatua za kisheria kwa wanachama na viongozi wa vyama vya Upinzani wanaomdhalilisha mgombea wa chama hicho bwana Sioi Sumari kwa kuzichana,ama kusipaka wanja na kuchora herein masikioni katika picha za mgombea huyo na kisha kuzibadika mitaani
Mratibu wa kampeni za chama hicho na mbunge wa Simanjiro Mheshimiwa Christofa ole Sendeka amesema vitendo hivyo vinaweza kusababisha machafuko endapo wafuasi wa chama kinocho tendewa hayo wakiamua kujibu mapigo kwa kuwa wanaofanya hivyo wanafahamika.