MBUNGE MTEULE WA ARUSHA MJINI GODBLES LEMA AVULIWA UWAKILISHI
Imeandikwa na Julius Laizer
Mahakama kuu Mkoani Arusha imemvua Ubunge Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na kutoa tamko la kurudiwa kwa uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo .
Akitoa hukumu hiyo jaji Gabrieli ameamuru uchaguzi huo kurudiwa kwa muda wa siku tisini kutokana na Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Godbless Lema kupatikana na hatia ya kutoa matusi pamoja na kumdhalilisha kijinsia aliyekuwa mgombea wa Jimbo hilo la Arusha batilda Buriani .
Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wananchi wa Jimbo hilo la Arusha wameonesha kusikitishwa na uamuzi huo wa mahakama kwani walimwamini mbunge wao kwa yale aliyokuwa akiyatenda
Lema amewataka wananchi wa jimbo la Arusha kutokuwa na vurugu katika jimbo hilo badala yake wakae na kutulia kwani wanaamini kuwa Chama cha demokrasia na maendeleo kitaendelea kutawala katika jimbo hilo
Kwa upande wake mwenyekiti wa Vijana CCM mkoani Arusha James Olemilia amesema kuwa siyo wakati wa Kufurahia wala kulalamika bali ni wakati ambao kila mmoja anatakiwa atafakari pale alipokosea pamoja na kuangalia wanapaswa kufanya nini .
No comments:
Post a Comment