Monday, April 2, 2012

Imeandikwa na  Julius Laizer
 DEMOKRASIA YA KWELI NI KUKUBALI MATOKEOO
Wananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki leo wanapiga kura katika uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuziba nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi na Jeremiah Sumari, ambaye alifariki dunia Januari.

Kinyang’anyiro cha kugombea nafasi hiyo kilichukua takribani mwezi mmoja ambapo vyama vinane vilijimwaga katika uwanja wa ushindani wa kisiasa na kueleza sera zao kwa staili ya kipekee, huku kila chama kikivutia upande wake.

kampeni hizo kulikuwa na vibweka vya kisiasa hasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) hakika kampeni hizo zinaonesha kiwango kikubwa cha ukomavu katika siasa nchini.

Mambo makuu yanayoonesha ukomavu wa demokrasia ni uhuru, haki, ushirikishwaji wa
wananchi, ushindani wa vyama vingi vya siasa, amani, utulivu na huru wa vyombo vya habari katika kufuatilia na kuripoti juu ya mchakato mzima wa uchaguzi.

Wakati wa maandalizi ya awali tulishuhudia vyama vikijitokeza na kupewa haki ya kushiriki katika uchaguzi huo.

Ndani ya chama kikongwe cha CCM uchaguzi wa kuteua mgombea ulirudiwa ili kuondoa manung’uniko na kuhakikisha kuwa demokrasia imefuata mkondo wake.

Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imetoa fursa kwa wananchi wenye sifa ya kupiga kura kujiandikisha ili kushiriki uchaguzi wa leo.

No comments:

Post a Comment