Tuesday, April 3, 2012

MBUNGE MTEULE JOSHUA NASARRI ACHIMBA VISIMA VIWILI

Imeandikwa na Julius Laizer

ARUMERU

Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Joshua Nassari, amemshukuru Mungu kwa kumwezesha kuwa mbunge na kukishukuru chama chake na wapiga kura kwa kumchagua kuliwakilisha jimbo hilo

Nassari ameyasema hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa hati na kutambuliwa rasmi kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo, kwa kushinda uchaguzi mdogo uliofanyika juzi na kushinda kwa aslimia 54 dhidi ya asilimia 42 alizopata mgombea mwenzake wa chama cha mapinduzi  

Mbunge huyo mteule ambaye ataapishwa Aprili 10 Dodoma, amewashukuru polisi kwa kufanya kazi kubwa ya kusimamia ulinzi wakati wote wa kampeni na wakati wa upigaji kura.

Amemwomba Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru, kuwaachia huru wapenzi wa chama hicho waliokamatwa kwa madai ya kufanya fujo na mikusanyiko.

Leo ameanza kazi ya kuchimba visima viwili vya maji katika Kata ya Maroroni. Amewahimiza wafuasi kujitokeza kwa wingi kufanya kazi hiyo ambayo tayari amekwishapewa fedha kwa ajili hiyo kutoka kwa Mbunge wa Moshi Vijijini, Philemon Ndesamburo (Chadema).

No comments:

Post a Comment