ARUMERU
O2/04/2012
Na
Jackson Mollel
Tume ya taifa ya uchaguzi imemtangaza mgombea
wa chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema bwana Nasari Joshua kuwa mbuge wa jimbo
la Arumeru mashariki.
Bwana Nasari aliye ingia katika kinyang`anyiro cha Ubunge
na wagomea wengine saba wa vyama mbalimbali ili kujaza nafasi ilio wachwa wazi na marehemu
Jaremia Solomon Sumari wa CCM aliyefariki dunia mapema Januari aliibuka mshindi
kwa kura 32,472 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Sioi Sumari wa Chama Cha mapinduzi aliyepata
kura 26,757
Mara baada ya msimamizi wa Uchaguzi huo bawana
Kagenzi kumtangaza mheshimiwa Nasari kuwa
mbunge wa Jimbo hilo, awali alimshukuru
mwenyenzi Mungu kwa yeye kupata nafasi hiyo vilevile wakazi wa Arumeru kwa wao kuchagua
kuwa mwakilishi katika bungeni la Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania.
Muheshimiwa Nasari amesema kuwa kwa ushindi
alioupata Arumeru Mashariki ni Ishara tosha ya Ushirikian na wakazi
wa Arumeru i katika kutekeleza ahadi
alizozitowa wakati wa kampeni zake jimboni humo.
Akizungumza na wana habari punde baada ya kutangazwa
kwake,mheshimiwa Nasari ametoa shurani
za zdhati kwa Jeshi la Polisi, kwa ulinzi na usalama katika
mchakato huo na kumtaka kamanda wa Polis
mkoani Arusha bwana Tobias Andegenye kuwaachia vija wote aliowakamata siku ya
Uchaguzi ili kusheherekea Ushindi wake.
By J.M Mollel.
No comments:
Post a Comment