Na Wilberd Kiwale
Simanjiro-Manyara
Hili ni basi la Coast line ambalo limepata ajali leo Juma mosi asubuhi katika kijiji cha Terrat kilichopo wilayani Sianjiro Mkoani Manyara,likitokea Arusha likielea Dodoma.
Zaidi ya abiria hamsini
wamenusurika kufa baada ya basi la kampuni ya Coast line walilokua wakisafiria kutoka mkoani Arusha
kuelekea Mkoani Dodoma kupasuka
tairi na kugonga mti katika kijiji cha
Terrat Wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Dereva wa gari hilo aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani Musa ambaye amevunjika mguu amesema Ajali hiyo
imetokea ghafla baada ya moja ya
magurudumu ya mbele ya basi hilo kupasuka wakiwa katika mteremko hali
iliyomfanya kushindwa kuhimili usukani na kugonga mti uliokuwa pembeni mwa bara bara hiyo.
Hawa ni baadhi ya abiria walionusurika katika Ajali hiyo
Na huu ndio mti wa Mgunga ambao Basi hili la COAST LIME limeugonga baada ya Kupasuka magurudumu ya mbele.
No comments:
Post a Comment