Sunday, April 29, 2012

AJALI YA COAST LINE

Ajali ya basi la kampuni ya Coast Line linalofanya safari yake kutoka arusaha kupitia Simanjiro,Kitento hadi Dodoma jana katika kijiji cha Terrat wilayani simanjiro mkoani manyaara.baada ya kugoga mti ulioko kando ya barabara

 by Jackson Mollel o.r.s fm

Saturday, April 28, 2012

BASI LA LA COAST LINE LAPATA AJALI MKOANI MANYARA LIKITOKEA ARUSHA KWENDA DODOMA


Na Wilberd Kiwale
Simanjiro-Manyara


Hili ni basi la Coast line ambalo limepata ajali leo Juma mosi asubuhi katika kijiji cha Terrat kilichopo wilayani Sianjiro Mkoani Manyara,likitokea Arusha likielea Dodoma.



Zaidi ya abiria hamsini wamenusurika kufa baada ya basi la kampuni ya Coast line  walilokua wakisafiria kutoka mkoani Arusha kuelekea Mkoani Dodoma   kupasuka tairi  na kugonga mti katika kijiji cha Terrat Wilayani Simanjiro  mkoani Manyara.

Dereva wa gari hilo  aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani Musa  ambaye amevunjika mguu amesema Ajali hiyo imetokea  ghafla baada ya moja ya magurudumu ya mbele ya basi hilo kupasuka wakiwa katika mteremko  hali  iliyomfanya kushindwa kuhimili usukani na kugonga  mti uliokuwa pembeni mwa bara bara hiyo.



           Hawa ni baadhi ya abiria walionusurika katika Ajali hiyo

 

Na huu ndio mti wa Mgunga ambao Basi hili la COAST LIME limeugonga baada ya Kupasuka magurudumu ya mbele.

Friday, April 6, 2012


MBUNGE MTEULE WA ARUSHA MJINI GODBLES LEMA AVULIWA UWAKILISHI

Imeandikwa na Julius Laizer

Mahakama kuu Mkoani  Arusha imemvua Ubunge Mbunge wa Arusha  mjini  Godbless Lema  na kutoa tamko la kurudiwa kwa uchaguzi  wa ubunge katika jimbo hilo .
Akitoa hukumu hiyo jaji Gabrieli ameamuru uchaguzi huo kurudiwa kwa muda wa siku tisini kutokana na  Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Godbless Lema kupatikana na hatia ya kutoa matusi pamoja na kumdhalilisha kijinsia aliyekuwa mgombea wa Jimbo hilo la Arusha batilda Buriani .
Wakizungumza kwa nyakati Tofauti wananchi wa Jimbo hilo la Arusha wameonesha kusikitishwa na uamuzi huo wa mahakama kwani walimwamini mbunge wao kwa yale aliyokuwa akiyatenda
Lema  amewataka wananchi wa jimbo la Arusha kutokuwa na vurugu katika jimbo hilo badala yake wakae na kutulia kwani wanaamini kuwa Chama cha demokrasia na maendeleo kitaendelea kutawala katika jimbo hilo
Kwa upande wake mwenyekiti wa Vijana CCM mkoani Arusha James Olemilia amesema kuwa siyo wakati wa Kufurahia wala kulalamika bali ni wakati ambao kila mmoja anatakiwa atafakari pale alipokosea pamoja na kuangalia wanapaswa kufanya nini .

Tuesday, April 3, 2012

MBUNGE MTEULE JOSHUA NASARRI ACHIMBA VISIMA VIWILI

Imeandikwa na Julius Laizer

ARUMERU

Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Joshua Nassari, amemshukuru Mungu kwa kumwezesha kuwa mbunge na kukishukuru chama chake na wapiga kura kwa kumchagua kuliwakilisha jimbo hilo

Nassari ameyasema hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa hati na kutambuliwa rasmi kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo, kwa kushinda uchaguzi mdogo uliofanyika juzi na kushinda kwa aslimia 54 dhidi ya asilimia 42 alizopata mgombea mwenzake wa chama cha mapinduzi  

Mbunge huyo mteule ambaye ataapishwa Aprili 10 Dodoma, amewashukuru polisi kwa kufanya kazi kubwa ya kusimamia ulinzi wakati wote wa kampeni na wakati wa upigaji kura.

Amemwomba Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru, kuwaachia huru wapenzi wa chama hicho waliokamatwa kwa madai ya kufanya fujo na mikusanyiko.

Leo ameanza kazi ya kuchimba visima viwili vya maji katika Kata ya Maroroni. Amewahimiza wafuasi kujitokeza kwa wingi kufanya kazi hiyo ambayo tayari amekwishapewa fedha kwa ajili hiyo kutoka kwa Mbunge wa Moshi Vijijini, Philemon Ndesamburo (Chadema).

CHADEMA WANYAKUA ARUMERU MASHARIKI

ARUMERU O2/04/2012
          Na Jackson Mollel
 Tume ya taifa ya uchaguzi imemtangaza mgombea wa chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema bwana Nasari Joshua kuwa mbuge wa jimbo la Arumeru  mashariki. 

Bwana Nasari aliye ingia katika kinyang`anyiro cha Ubunge na wagomea wengine saba wa vyama mbalimbali ili  kujaza nafasi ilio wachwa wazi na marehemu Jaremia Solomon Sumari wa CCM aliyefariki dunia mapema Januari aliibuka mshindi kwa kura 32,472 dhidi ya mpinzani wake wa karibu  Sioi Sumari wa Chama Cha mapinduzi aliyepata kura 26,757   

Mara baada ya msimamizi wa Uchaguzi  huo  bawana Kagenzi kumtangaza mheshimiwa  Nasari kuwa mbunge wa Jimbo hilo,  awali alimshukuru mwenyenzi Mungu kwa yeye kupata nafasi hiyo  vilevile wakazi wa Arumeru kwa wao kuchagua kuwa mwakilishi  katika bungeni  la Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania.

Muheshimiwa Nasari amesema kuwa kwa ushindi alioupata  Arumeru Mashariki  ni Ishara tosha ya Ushirikian   na wakazi wa Arumeru i katika  kutekeleza ahadi alizozitowa wakati wa kampeni zake jimboni humo.

Akizungumza na wana habari punde baada ya kutangazwa kwake,mheshimiwa Nasari  ametoa shurani za  zdhati  kwa Jeshi la Polisi, kwa ulinzi na usalama katika mchakato huo na kumtaka  kamanda wa Polis mkoani Arusha bwana Tobias Andegenye kuwaachia vija wote aliowakamata siku ya Uchaguzi ili kusheherekea Ushindi wake.
                                                    By J.M Mollel.

Monday, April 2, 2012

Imeandikwa na  Julius Laizer
 DEMOKRASIA YA KWELI NI KUKUBALI MATOKEOO
Wananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki leo wanapiga kura katika uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuziba nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi na Jeremiah Sumari, ambaye alifariki dunia Januari.

Kinyang’anyiro cha kugombea nafasi hiyo kilichukua takribani mwezi mmoja ambapo vyama vinane vilijimwaga katika uwanja wa ushindani wa kisiasa na kueleza sera zao kwa staili ya kipekee, huku kila chama kikivutia upande wake.

kampeni hizo kulikuwa na vibweka vya kisiasa hasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) hakika kampeni hizo zinaonesha kiwango kikubwa cha ukomavu katika siasa nchini.

Mambo makuu yanayoonesha ukomavu wa demokrasia ni uhuru, haki, ushirikishwaji wa
wananchi, ushindani wa vyama vingi vya siasa, amani, utulivu na huru wa vyombo vya habari katika kufuatilia na kuripoti juu ya mchakato mzima wa uchaguzi.

Wakati wa maandalizi ya awali tulishuhudia vyama vikijitokeza na kupewa haki ya kushiriki katika uchaguzi huo.

Ndani ya chama kikongwe cha CCM uchaguzi wa kuteua mgombea ulirudiwa ili kuondoa manung’uniko na kuhakikisha kuwa demokrasia imefuata mkondo wake.

Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imetoa fursa kwa wananchi wenye sifa ya kupiga kura kujiandikisha ili kushiriki uchaguzi wa leo.