TERRAT
SIMANJIRO-20120702Swaa.doc.jumanne
Semina ya siku
mbili ya mafunzo elekezi ya upashanaji habari za kijamii imeanza leo katika
ukumbi wa mikutano wa taasisi ya shirika la Ilaramatak lorkonerei uliopo Terrat
Simanjiro mkoani Manyara
Wakizungumzia
lengo la mafunzo hayo wawezeshaji ambao ni bwana Moses Ndiyaine na Lucas Ole
Kariongi wamesema jamii inapaswa kutambua na kupata fursa ya kuchangia
maendeleo yao
katika kila jambo linalo wahusu
Mafunzo hayo yanawalenga
watumishi wa Orkonerei Mass Media na wanahabari wote wa O.r.s fm kwa lengo la kufanikisha majukumu yao ya kila siku ya
kuhabarisha jamii juu ya mambo mbali mbali yanayotekea katika jamii hapa
nchini.
Wawezeshaji hao
wamewataka wanahabari kuandika habari mbali mbali za jamii ikiwamo unyanyasaji
wa wanawake upatikanaji wa huduma muhimu kama
hospitali shule bara bara na masuala yanayo wahusu watoto na haki zao
Mafunzo haya yanawanufaisha vipi
ReplyDelete