ORBOMBA-LONGIDO 20/02/2012,
Na Baraka Ole Maika.
Vijana wa Rika la Irkiponi maarufu kama Korianga Wilayani Longido wamemzawadia Kiongozi wao wa Mila Alaiguanani Sarimu Alais Pikipiki yenye thamani ya Shilingi Milioni tatu kama usafiri utakaomrahisishia utendaji wake wa Kazi kila siku.
Wakiongea na Waandishi wa Habari Mara baada ya Kumkabidhi Kiongozi huyo Pikipiki Mmoja wa Waratibu wa Ununuzi wa Pikipiki hiyo Bw Sonjoi Ole Ndiya amesema kuwa wameamuwa kumnunulia Kiongozi huyo pikipiki kama ishara ya Mema aliowatendea,kuthamini Mchango na Uongozi wake Uliotukuka.
Aidha Bw Sonjoi amesema kuwa waliridhia hatua hiyo ya kumnunulia Alaiguanani Pikipiki ili aweze kupata Usafiri wa uhakika wa kufikia Maeneo yake yote ya Utendaji kwa Wakati kwa kutumia Usafiri wake huo hivyo kuondokana na tatizo la Usafiri ambao ulikuwa unamkwamisha kufika katika Vikao kwa wakati.
Bw Sonjoi amesema kuwa pamoja na Kiongozi huyo ktokuwa na Usafiri kwa Siku za nyuma lakini hajawahi kulalamika wala kukataa tamaa kuhudhuria Vikao mbali mbali zinazohusu rika lake na hata jamii bali wakati mwingine alilazimika kutumia gharama zake bila kujali Umbali wala Mazingira.
Aliyemkabidhi Kiongozi huyo Pikipiki kwa Niaba ya Irkiponi wote ni Bw Joseph Lankoi Ole Niini ambaye aliwashukuru sana Vijana hao kwa Tendo hilo ambalo linaonesha kuwa nao wanayathamini yale yote Mema waliotendewa na Kiongozi hiyo wa Mila.
Bw Ole Niini aliwaasa Pia Viongozi na Rika hilo la Irkiponi kudumisha Umoja,Upendo na Ushirikiano pamoja na kusaidiana na hata kuwarejesha wale wote waliotoweka na kukimbilia Mijini.
Bw Ole Niini pia alitoa kiasi cha shilingi Laki 1 ikiwa ni Mchango wake kwa ajili ya Mafuta ya Piki piki hiyo.
Awali kabla ya Alaiguanani kukabidhiwa Piki piki hiyo alibarikiwa na Wazee Mashuhuri na pamoja viongozi wa Mila ikiwa ni tukio la pili baada ya Kiongozi huyo Kunywa Maziwa Usiku pamoja na Morani Wengine zaidi ya 30.
Mara baada ya Tukio la kukabidhiwa piki piki kukamilika Wazee waliwabariki Vijana wote kwa Maziwa ishara ya kuwatakia Mema na Baraka katika Maisha yao.
Alaiguanani Sarimu Alais aliwashukuru sana wote waliohusika katika kumpatia yeye Piki piki japo hakuwahihusita wala kuchoka kutenda yale yote yalio Majukumu yake hata kwa gharama zake na kuahidi kuwa sasa ndio atatenda kwa Ufanisi Zaidi tofauti na Awali.
Alaiguanani Sarimu ni Kiongozi wa Kwanza wa Mila kuzawadiwa Zawadi ya Usafiri(Piki piki) na Rika lake kwani tukio kama hilo haijawahi kutokea kwa Miaka ya nyuma zaidi ya Kuzawadiwa Ng'ombe,Mbuzi,Kondoo au Blanket.
No comments:
Post a Comment