Monday, February 20, 2012

LONGIDO,19/02/2012.
Na Baraka Ole Maika.


Rais Jakaya Kikwete amezindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa Kaya zilizoathiriwa na Ukame Msimu wa 2008/2009 na 2009/2010 katika Wilaya za Longido,Monduli na Ngorongoro.


Uzinduzi wa Mradi huo utakaogharimu shilingi 11.2 Bilioni ulifanyika katika Uwanja wa Mnadani Wilayani Longido Mkoani Arusha na Kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Mila Chama na Serikali pamoja na Wakazi wa Wilaya ya Longido waliofurika kwa Wingi katika Eneo hilo kushuhudia tukiohilo la Kihistoria.


Akihutubia hadhara hiyo Rais Kikwete aliliwataka Wafugaji wa Longido na Wilaya Zingine zitakazonufaika na Mradi huo kutambua kuwa hiyo sio fidia ila ni huruma tu ya Serikali kwa hakuna aliyesababisha Ukame ulioteketeza Mifugo hao ya Wafugaji.

Aidha Rais Kikwete aliwakabidhi Mifigo hao baadhi ya Waathirika kutoka Kata 16 na kuiwaasa Wafugaji kuwa wajifunze kufuga Mifugo wachache wenye Tija kwao na wataomudu kuwahudumia kulingana na Maeneo waliopo na pia kwa kuangalia hali ya Mazingira na Maeneo waliopo.

Pamoja na Hayo Rais Kikwete aliawataka Wananchi hao washiriki kikamilifu katika Zoezi la Sensa ya Watu litakalofanyika August'2012 na kujiokeza kwa wingi katika utoaji Maoni ya Kuunda Katiba Mpya inayotarajiwa kukamilika kabla ya Mwaka 2015.

Kuhusu tatizo la Maji katika Wilaya ya Longido hasa Longido Mjini Rais Kikwete aliwaomba Wakazi hao wawe na subira wakati akilitafutia ufumbuzi tatizo hilo.


Rais Kikwete pia aliwaasa Wafugaji wote waliopata Mifugo kupitia Mradi huo kutotumia Mifugo hao kwa Matumizi yaliyo kinyume na Lengo lililokusudiwa.


Naye Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh Mathayo David aliwaeleza Wananchi hao Mikakati ya Serikali katika kuboresha Uboreshaji wa Mifugo ili ziweze kuleta tija kwa Mfugaji kwa ndio njia pekee ya Kiuchumi inayotegemewa na Wafugaji.


Viongozi Mbalimbali walioandamana na Mh Kikwete katika Ziara yake hiyo ni Pamoja na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mh Wilium Lukuvi,Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh Mathayo David,Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh Benedict Nangoro,Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowasa,Saning'o Telele(Ngorongoro),Mbunge wa Karatu na Mbunge wa Longido Mh Michael Lekule Laizer.


Wengine walioshudia Uzinduzi wa Mradi huo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo,Mkuu wa Wilaya ya Longido Jamsi Milya,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mercy Silla,Mkuu wa Wilaya ya Monduli Jowika Kasunga,Mkuu wa Wilaya ya Karatu Sedeyeka na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Wawa Lali.


Mradi huo wa kuwawezesha Wafugaji waliopoteza Mifugo yao wakati wa Ukame 2008/2009 ni wa Kwanza kufanyika Tanzania na utanufaisha kaya Zaidi ya Elfu 7 kutoka Wilaya za Longido,Monduli na Ngorongoro kwa kila kaya kupatiwa Mitamba minne na Dume moja isipokuwa Wilaya ya Longido ambao wao wameomba wapatiwe Mitamba Mitano,ila Pamoja na Mitamba hiyo kuna baadhi ya Kaya watapatiwa Mbuzi watano.

No comments:

Post a Comment