Friday, February 17, 2012
Longido leo Jioni.
Longido.
Na Mwandishi wetu,
Baraka Ole Maika.
Kiongozi wa Rika la Irkiponi(Korianga) Wilayani Longido Alaiguanani Sarimu Alais atawaongoza Vijana zaidi ya 40 wa rika hilo katika sherehe ya kunywa Maziwa(Ewokoto E kule) siku ya Leo Jioni katika Kitongoji cha Emamra Kijiji cha Orbomba Wilayani Longido.
Sherehe hiyo inatazamiwa kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Mila,Chama na Serikali kutoka Maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Longido na Maeneo ya Jirani.
Alaiguanani Sarimu atasindikizwa na Vijana zaidi ya 40 wa Rika la Irkiponi katika Unywaji wa Maziwa ikiwa ni hatua Muhimu kwa Kila Rika ndani ya Jamii ya Kimaasai ambayo inatoa Fursa kwa Kiongozi wa mila na Rika lake kuingia katika Maandalizi ya Kuelekea Uzeeni(Orng'ehher) na Kuwapa Madaraka Rika Jipya la Iltubula almaarufu kama Nyangulo.
Hatua hii inafikiwa kila baada ya Miaka 15 hadi 20 ambapo Rika la Vijana lililokuwa Madarakani linaachia nafasi Rika jipya lililoandaliwa kwa Miaka 20 iliyopita tayari kupokea madaraka ya Ulinzi na Usalama wa Jamii na Mifugo yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment