Na Baraka Ole Maika.
Mgogoro wa kugombania Kitongoji cha Katikati baina ya Kijiji cha Sukuro na Kitiengare Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara imechukuwa sura mpya wakati wa Ziara ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh George Huruma Mkuchika.
Hali ya Mtafaruku iliibuka pale Waziri Mkuchika alipoelezea kuwa Kitongoji cha Katikati kinapaswa kupiga kura na kuchagua kuwa iwepo kwenye Kijiji gani Kati ya Sukuro(Kijiji Mama) na Kitiengare(Kijiji kipya) tofauti na Awali ambapo Kitongoji hicho kilikuwa Kijiji ch Sukuro katika Taarifa iliyotolewa na TAMISEMI 2009 na kusomwa Kijijini Sukuro na aliyekuwa Mkuu wa Manyara Henry Daff Shekifu.
Taarifa hiyo ya Waziri Mkuchika iliibua hali ya taharuki na Makelele kutoka kwa wakazi wa Vijiji hivyo viwili ambao walikuwa wakimtaka Mh Waziri kutolea Maamuzi Jambo hilo kwani ndio njia pekee ya kuondoa Mvutano huo uliodumu kwa Muda sasa Kijijini hapo.
Kelele za Wakazi hao zilibainisha kuwa ni ni vema Waziri Mkuchika atolee Maamuzi jambo hilo kwani anayewavuruga na kuwakosesha usuluhishi ni Mh Christopha Ole Sendeka kwa maslahi yake Binafsi na amekuwa akifanya ziara zake Kijijini hapo pindi tu Viongozi wa Ngazi za Juu wanapofika Katika Kijiji hicho cha Sukuro.
Kelele hizo zilimfanya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo asimame na kuwaomba wananchi hao kufuata Maelekezo waliopewa kwani Ugawanyaji wa Vijiji sio Msahafu wala Biblia ambayo haibadilishi ila Wakazi wa Kitongoji cha Katikati wakapige kura ya Kuamua kuwa waende Kijiji gani.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara aliwaelekeza wakazi hao kuwa Maamuzi yao yote yaanzie Mkutano Mkuu wa Kitongoji halafu Mkutano wa Kijiji,Mkutano wa Kata(WDC),Baraza la Madiwani na Hatimae Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC).
Naye Waziri Mkuchika aliwaeleza wananchi hao kuwa Mchakato huo unapaswa uwe umekamilika kabla ya Mwezi wa April na kupelekwa Ofisini kwa Waziri Mkuu.
Wakazi hao pia walimkataa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Khalid Mandia na Mbunge Ole Sendeka kuhusika katika Mchakato huo kwa kile kinachodaiwa kuwa walishindwa tangu Mwanzo kuutatua Mgogoro huo na Sendeka ndiye Mchochezi Mkuu.
Kutokana na Kauli hiyo ya Wakazi hao Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo alimpendekeza Mkurugenzi wa Wilaya ya Simanjiro Alhaji Mohammed Nkya pamoja wa wengine atakaowateuwa kutoka Ofisini kwake kusimamia Zoezi hilo la Upigaji kura katika Kitongoji cha Katikati.
Hali kwa kweli bado ni tete katika Vijiji vya Sukuro na Kitiengare Juu ya Kitongoji hicho cha Katikati kwani hapo awali Kitongoji hicho kilikuwa Kijiji cha Sukuro ila Wakazi wa Kitongoji hicho waligawanyika na kutokea makundi mawili ambao ni wale walioridhia kubaki Sukuro na Kundi la wale wanaotaka wawe Kitiengare.