Saturday, October 6, 2012

STAKEHOLDERS MEETING BETWEEN ORMAME, GOVERNMENT OF TANZANIA AND CIVIL SOCIETY ORGANIZATION - IOPA OFFICE ARUSHA

Stakeholders meeting between Government of Tanzania (Prime Minister's Office, Ministry of Livestock and Fisheries, Ministry of Lands) CSO's (IOPA, Oxfam, NGONET,ICS)

 OMASI & IOPA General Director Martin Saning'o Kariongi during the Introduction session held in IOPA Offices - Arusha.

 Associate Country Director from Oxfam - Justin Morgan (left) and Coordinator of NGONET from Ngorongoro District Mr. Samweli Nangiria was one of the participants in the Meeting.

 Research and Development General Manager - OMASI Mr. Lazaro Ole Mongoi (left) and Leo M. Mavika from Prime Minister's Office, Regional Administration and Local Government Sector Coordination Department, listens to ORMAME General Director Mosses Ndiyaine (not in the photo) during the Stakeholders Meeting.


 Roine Megirori a Programme Officer from Ilaramatak Lorkonerei Institute - IOPA heading a Livelihood Programme under IOPA.


The General Director of Orkonerei Mass Media - ORMAME, presenting a lesson learnt during their visits to see the communities and Organization working to secure rights to resources and land for rangeland users in Kenya and Tanzania.



 ORMAME Programme Director Lukas Kariongi, followup the session.


 Mr. Deusdedit M. Kalenzi - Director of Research and Documentation from National Land Use Planning Commission - DSM follow up the session during the stakeholders meeting.


 Mr Samwel Leshongo from Ministry of Livestock and Fisheries Development DSM is among the people from the government attending the stakeholders meeting.

 An Amalgamation of International Organizational supported and Invited 22 Participants from 13 Countries went to a Learning route to see the communities and organization working to secure rights to resources and land for rangeland users in Tanzania and Kenya.

Places visited are Laikipia District, Magadi and Gabra region of Kenya; and in Tanzania participants visited Terrat village.

The ultimate goal of the visit is for COS's and Government participants in respective countries is to learn from each other and from cases and provide workable solutions for security of rangeland users mainly pastoralists.

During their stays they observe that; Migratory Pastoralism is an adaptive  production strategy assuring the economic survival of hundreds of millions of people, as well as a way of life contributing to the sustainable management of natural resources and the conservation of nature.

Participants of Tanzania also learnt that countries governments have "nationalised" and confiscated rangelands, forests and other natural resources on which pastoralists depend, removing them from community care, control and property and alienating nomadic pastoralists from their natural rights. In the meantime, current neoliberal economic and social policies globally impose the privatization of natural resources - including life itself.

Regarding to that participants from Tanzania agreed that CSO's and the government needs to formulate a National project as matter of priority that facilitates and make rangeland secure for  pastoralists use throughout the country. And these is the result of stakeholders meeting with Governments officials from Prime ministers office (Ministry of Livestock and Fisheries, Ministry of Lands) CSO's (IOPA, Oxfam, NGONET,ICS) with the objectives of 
1. PROVIDE the necessary policy support to achieve the economic and social development in harmony with nature.
2. DEVELOP strategies and mechanisms to support pastoralists to reduce the impact of droughts and climatic change.
3. PROVIDE adequate and appropriate veterinary services, assuring that relevant animal diseases are promptly addressed for prophylaxis and treatments, as well as in action - research.
4. ADOPT measures to reverse negative environmental impacts of development schemes, and seek prior and informed consent before all private and public initiatives that may affect the integrity of pastoralists people's customary territories, resource management systems and nature.
5. Develop mechanism for broader rangeland use for pastoralism by supporting initiatives for access, control and ownership of lands for pastoralists.
6. SUPPORT the strengthening of the organizations of pastoralists at national, regional and international levels, including through the promotion of programs to disseminate relevant knowledge on rights and policy among pastoral and other mobile communities.
7. RECOGNIZE the crucial role of indigenous knowledge and the capacity of pastoralists and all other nomadic and transhumant communities to conserve biodiversity in full compatibility with pastoral livelihoods; EMPOWER mobile communities in the management of existing protected areas and, RECOGNIZE their customary territories as community conserved areas (CCAs) when so demanded by the concerned mobile peoples and communities;
8. PROMOTE conditions and mechanisms for lasting peace and conflict resolution at all levels;
9. PROMOTE control of markets with policy, incentives, infrastructure development, capacity building and access to information, in order to achieve fair trade conditions.

Friday, August 31, 2012

MSIMAMO WA MASHIRIKA YA KIRAIA NA MTAZAMO WA AVAAZ KUHUSU KUTAKA SERIKALI KUSIMAMISHA MCHAKATO WOWOTE WA KUUZA ELEO LA LOLIONDO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA AMBAYO NI ARDHI YA VIJIJI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA HII INATOLEWA NA MASHIRIKA YA KIRAIA KUELEZEA MSIMAMO WAO KATIKA KAMPENI INAYOENDESHWA NA MTANDAO WA AVAAZ KUHUSU KUTAKA SERIKALI KUSIMAMISHA MCHAKATO WOWOTE WA KUUZA ENEO LA LILIONDO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA YA SERENGETI UPANDE WA MASHARIKI AMBAYO NI ARDHI YA VIJIJI

SISI mashirika ya kiraia yanayofanya kazi nchini Tanzania katika masuala ya haki za binadamu, uchumi wa kijamii, ikiwa ni pamoja na ardhi, usawa wa kijinsia, mazingira na rasilimali kwa jumla tunaunga mkono kampeni inayoendeshwa na mtandao wa kimataifa wa Avaaz ambao ni ulingo wa kimtandao unaotetea haki za binadamu kwa njia ya matamko mbalimbali. Mtandao huu umetoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusitisha mpango wowote wa kuuza ama kutoa sehemu ya ikolojia ya mashariki ya hifadhi ya Serengeti ambayo ni makazi ya wafugaji wa Kimaasai katika wilaya ya Ngorongoro, tarafa ya Loliondo kwa kampuni ya uwindaji wa wanyama pori ya OBC. OBC ni kampuni ya uwindaji inayomilikiwa na familia ya kifalme ya Ufalme wa Umoja wa nchi za Kiarabu (United Arabs Emirates - UAE). Itakumbukwa kuwa mitandao ya Tanzania Land Alliance (TALA) na FEMACT imekuwa ikijishughulisha na migogoro ya Loliondo kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kutoa matamko mbalimbali. Hata hivyo, serikali imekuwa ikisita kutekeleza mapendekezo hayo.

Mgogoro wa Loliondo umekuwepo kwa takriban miaka 20 tangu mwaka 1992 lakini ilifikia kilele mwaka 2009 ambapo serikali iliwatoa kwa nguvu wafugaji wa kimaasai katika eneo la ikolojia ya Serengeti upande wa mashariki kwa lengo la kuanzisha korido au mapito ya wanyama pori katika eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,500 ambalo ni ardhi ya vijiji saba (7) vya Loliondo. kwa kuanzishwa kwa mapito ya wanyama katika enelo hilo, maisha ya watu takriban 48,000 yataathirika na mifugo mingi pia.

HISTORIA FUPI YA UWEKEZAJI KATIKA ENEO LA MGOGORO, LOLIONDO

Tangu eneo la Loliondo ambalo ni eneo la ikolojia ya Serengeti kwa upande wa mashariki kupewa mwekezaji wa Kiarabu ambaye ni familia ya Kifalme kutoka nchi za Umoja wa Kifalme za Kiarabu kupitia kampuni ya OBC (Otterlo Business Corporation) mwaka 1992, eneo la Loliondo liliendelea kuwa na mgogoro baina ya vijiji kwa upande mmoja na OBC na serikali kwa upande wa pili. OBC walipewa kibali cha uwindaji katika eneo lote la Tarafa ya Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro tangu mwaka 1992. Tangu wakati huo ambapo kampuni ya OBC inapewa kibali cha uwindaji, kulizuka upinzani wa wananchi kutokana na mchakato wa kumpa OBC eneo la kuwindia kutokuwa wazi na pia shirikishi. Kutokana na mapungufu haya baina ya serikali na OBC, ulizuka mgogoro ambao umeishi mpaka leo bila ufumbuzi. Hata hivyo, mwaka 2008 serikali wakishirikiana na OBC waliandaa mkataba na vijiji, mkataba huo ulitaka vijiji kuondoka kwa hiari katika eneo hilo ambalo OBC wameweka kambi yao ili kuweza kufanya uwindaji wa kibiashara. Katika mchakato huo wa mikataba, vijiji vingine vilikubaliana na vingine vikakataa. Kutokana na kutokubalika kwa mikataba hiyo kwa asilimia zote, serikali mwaka 2009 July iliazimia kuwatoa wamasai katika eneo hilo kwa nguvu jambo lililopelekea jamii ya wafugaji wa kimaasai kupata hasara kublwa ikiwa ni pamoja na kunyimwa kulisha na kunyesha mifugo yao katika eneo hilo. Tangu kumalizika kwa operesheni hiyo, serikali iliendelea kufanya michakato mbalimbali kuhusiana na eneo hilo yenye malengo ya kufanikisha azma yao ya kuhakikisha kuwa eneo hilo linatengwa kutoka katika ardhi ya vijiji na kuachwa chini ya Kampuni ya Kiarabu, OBC kwa ajili ya utalii wa Uwindaji.


MADHARA YATOKANAYO NA WANANCHI KUONDOLEWA KWA NGUVU LOLIONDO MWAKA 2009

Kutokana na operesheni ya kuwaondoa wananchi, wafugaji wa kimaasai katika ikolojia ya serengeti ilipitisha biashara ya uwindaji kwa kampuni ya OBC, wananchi waliathirika kwa kiasi kikubwa na yafuatayo ni baadhi tu ya madhara walioyapata;

  1. Usumbufu kwa wananchi;
  2. Zaidi ya nyumba za wamasai 350 zilichomwa mtoto na kuteketea kabisa;
  3. Zaidi ya watu 20,000 walikumbwa na mkasa huo na kuondolewa kwa nguvu,
  4. Zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya mifugo iliyokuwepo katika eneo hilo ilikufa kutokana na kukosa malisho ya kutosha na maji;
  5. Baadhi ya watoto walipotea wakati wa operesheni;
  6. Kuharibika kwa mimba za akina mama kutokana na hofu na mshtuko;
  7. Watu wengi kuchapwa na kudhalilishwa na kijana Ngodidyo Roriken alipigwa risasi ya jicho na kusababishiwa ulemavu wa jicho moja;
  8. Watu wengi walishitakiwa na kubambikiziwa kesi ya kuingia eneo la liliodaiwa la OBC angali ni eneo la vijiji.

HATUA ZILIZO CHUKULIWA NA SERIKALI BAADA YA OPERESHENI

Pamoja na operesheni kushindwa kuwaondoa wananchi katika eneo hilo, serikali iliendelea kuhakikisha kuwa inatimiza azma yake ya kutenga eneo hilo, kwa manufaa ya OBC. Baadhi ya michakato ambayo serikali iliendelea nayo baada ya operesheni ni pamoja na;

  • Kutuma tume mbalimbali kuchunguza mgogoro bila kutoa wala kueleza matokeo ya uchunguzi wa tume hizo kwa umma wala kwa mamlaka husika.
  • Mwaka 2010, serikali kupitia kwa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro iliandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya wilaya, mpango ambao ulilenga kutenganisha ardhi ya vijiji na eneo la ikolojia ya Serengeti na kuanzisha korido ya wanyama ambayo itakuwa ikitumiwa na OBC kuwinda wanyama. Mpango huu ulikataliwa na wananchi kupitia baraza la Madiwani, kwani haukuwa shirikishi na ulikuwa vigumu kuanzisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ya wilaya kabla ya mipango ya vijiji kutengenezwa.
  • Mwaka 2011, serikali iliandikia vijiji vyenye vyeti vya ardhi ya vijiji, vya Ololosokwan na Ngaresero barua na kuziraka kurudisha vyeti vyao ili kuvibatilisha kwa lengo la kufanikisha na kurahisisha uundaji  wa korido ya wanyama.
  • Kuanzishwa kwa mpango wa kuwatumia viongozi ndani ya jamii kuhamasisha jamii kuondoka ili kupisha serikali kuanzisha korido ya wanyama. Jamii kupitia mikutano yao vijiji vilikataa mpango huu baadhi ya viongozi kutumika na serikali na OBC kutaka kuwahamisha wananchi katika eneo hilo la ikolojia ambalo ndilo eneo la malisho ya mifugo kwa miaka mingi.
  • Kutokanaa na michakato hiyo yote kuonekana kushindikana, bado serikali haijatolea uamuzi mgogoro huu, jambo linalosababisha wananchi kuishi kwa hofu kubwa bila kufahamu hatima ya maisha yao.

MAPENDEKEZO

Kutokana na hayo, sisi mashirika yanayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania tunaunga mkono kampeni za mtandao wa kimataifa wa Avaaz na kuitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya yafuatayo:-

  1. Kuacha mara moja mpango wa kuigawa ardhi ya vijiji kwa ajili ya kuanzisha korido ya wanyama kwa malengo ya kuwanufaisha wawekezaji wa OBC.
  2. Serikali iandae mpango shirikishi wa matumizi bora ya ardhi utakao zingatia maslahi na mahitaji ya wanavijiji wote.
  3. Mikataba yote inayohusu shughuli za uwindaji katika eneo husika iangaliwe na kuridhiwa upya ili kuzingatia haki, matakwa na maslahi ya wananchi juu ya rasilimali husika.
  4. Mapendekezo ya Kamati na Tume mbalimblai ziliotembelea eneo hilo yawekwe wazi na kutekelezwa ili tija ya matumizi ya kodi za wananchi ionekane.
  5. Serikali iache tabia ya kutumia nguvu kila wakati kunapokuwa na mvutano ama mgongano wa maslahi kati ya wananchi wa wawekezaji.


TALA                                                            FEMACT


                                                                                                            


NGONET                                                       PINGOS FORUM


                                                                                                             

Thursday, August 9, 2012

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA MANYARA NA MKUU WA WILAYA YA SIMANJIRO KATIKA KIJIJI CHA TERRAT KUHAMASISHA JUU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA MANYARA NA MKUU WA WILAYA YA SIMANJIRO KATIKA UHAMASISHAJI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo kushoto, mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Supuk Nelukendo na kulia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Simanjiro Brown Ole Suya, wakati wa uhamasishaji wa sensa ya wati na makazi katika kijiji cha Terrat.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Terrat waliofika kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo na Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Kanali Cosmas Kayombo (hawapo pichani) kuhusiana na sensa ya watu na makazi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Supuk Nelukendo akiongea na wananchi, juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu wa 8 nchi nzima.
 Mwanyekiti wa CCM vijana kata ya Loiborsoit Lee Shinini akiuliza swali ili apate ufafanuzi juu ya kuhesabiwa kwa mifugo ya wafugaji ambayo ipo nje wilaya ya Simanjiro.
 Mwananchi wa kijiji cha Terrat Godson Nduya naye akiuliza swali ili aweze kupata ufafanuzi juu ya sensa ya watu na makazi.
Mzee wa kifugaji akimuuliza swali mkuu wa Mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo (hayupo pichani) kuhusiana na sensa ya watu na makazi.
 Afisa matangazo ya nje (PA) wa ORS FM Greyson Martin Orongai, akihakikisha kila kila kinachozungumzwa kinasikika kwa ufasaha kwa kutumia microphone na spika ziliwekwa katika uwanja wa mikutano.
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa ORS FM Baraka David Ole Maika aliyeshika microphone akirekodi yale yanayozungumzwa na Afisa Utamaduni wilaya ya Simanjiro Lameck Nanyaro wakati mkuu wa mkoa wa Manyara na Mkuu wa wilaya ya Simanjiro (hawapo pichani) walipofungua mafunzo ya wakufunzi wa sensa ya watu na makazi katika kijiji cha Terrat jana.


Katika ziara yake ya kutembelea wilaya ya Simanjiro na mkoa wa Manyara, Mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo ametoa hamasa kwa jamii ya kifugaji kujitokeza kushiriki katika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika tarehe 26/08/2012 kote nchini.

Pia amewataka kuachana na dhana iliyojengeka miongoni mwa wengi kuwa kuhesabiwa kwa watu au mifugo kunasababisha kifo.

Bwana Elasto Mbwilo ameitaka jamii ya kifugaji kuanza kulima kilimo chenye tija ili waweze kujihifadhia mazao kwa ajili ya chakula cha baadaye cha familia kuliko kubweteka na kusubiria chakula cha msaada, na ametilia mkazo kuwa mbali na mahindi pia wahakikishe wanapanda mazao yanayostahamili ukame kama vile Mtama na yeye yupo tayari kuwatafutia soko endapo kama watakosa pa kuuzia.


Imerushwa na: Khadija Abdallah
Picha kwa hisani ya Greyson Martin Orongai na Baraka David Ole Maika

Monday, July 9, 2012

ILIVYOKUWA AJALI YA COAST LINE

by Jackson Mollel.                     MAKALA KATIKA PICHA


AJALI YA BASI LA KAMPUNI YA COAST LINE 28/04/2012  HASUBUHI LINALOFANYA SAFARI KATI YA ARUSHA NA DODOMA KUPITIA WILAYA ZA SIMANJIRO NA KITERO









SHINA LA MGUGA ULIYOGONGWA NA BASI
ENEO LA AJALI KATIKA KIJIJI CHA TERRAT WILAYANI SIMANJIRO MKOANI MANYARA


KUSHOTO NI DREVA WA BASI HILO BWANA RAMADHANI ALIYEVUNJIKA MGUU WA KULIA NA MWINGINE KUPATA MAJERAHA MAKUBWA
MTOTO ALIYERUSHWA KUPITIA KIOO  CHA MBELE NA AKATOKA SALAMA BILA HATA JERHA LOLOTE


ABIRIAALIYEJULIKANA KWA JINA LO LOHANGA ALIPANWA KIFUA NA KUPATA MAJERAHA KICHWANI




WAUGUZI KATIKA ZAHANATI YA TERRAT WAKITOA HUDUMA YA KWANZA KWA MAJERUHI
BAADA YA HUDUMA YA KWANZA SAFARI ILIANZA KUELEKEA KIJIJI JIRANI CHA LOSWAKI KILIPO KIWANJA CHA NDEGE CHA FLYING MADICAL SERVICE KM SABAKUTOKA ILIPO ZAHANATI YA TERRAT MAJERUI WAPELEKWE  MJINI ARUSHA


MAJERUHI WAKIWA KWENYE  GARI LA TAASISI YA ILARAMATAK LORKONEREI LILILOWAPELEKA UWANJA MDOGO WA NDEGE KIJIJINI LOSWAKI

NDEGE YA FLYING MEDICAL SERVICE KATIKA KIJIJI CHA KOSWAKI DAKIKA KUMI NA SITA TANGU IMEITWA KUTOKA UWANJA WA NDEGE KISONGO MJINI ARUSHATAWARI KWA KUWAPELEKA MAJERUHI.



 
MAJERUHI LOHANGA AKIPATIWA HUDUMA NA PADRI RUBANI WA NDEGE YA FLYING MEDICAL SERVICE KABLA YA KUPAKIWA KWENYE NDEGE .
LUHANGA AKUPAKIWA KWENYE NDEGE KWA MSAADA WA WAKAZI WA KIJIJI CHA TERRAT NA OLOSWAKI MAJIRA YA SAA NANE MCHANA





                        

NA NDEGE IKAWA TAYARI KUONDOKA IKIWA MAJERUHI WOTE WAMEPAKIWA  KUELEKEA UWANJA MDOGO WA NDEGE KISONGO MKOANI ARUSHA


 

NA BAADAE TUKAREJEA TENA KATIKA ENEO LA TUKIO  




 

HUYU NI BABA WA MTOTO WA ALIYENUSURIKA AKIWA NA MWANAE











MAFUNDI SEREMALA MWANZA WALALAMIKIA HALI NGUMU YA MAISHA

Jackson Mollel

Imebainika kuwa hali ngumu ya maisha inayowakabili mafundi seremala wa jiji la mwanza inatokana na ungizwaji wa samani kutoka nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya mafundi hao walipozungumzaa na ors fm hili hivi karibuni, katika maeneo yao jijini humo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake bwana Inocent Mkumbo ambaye ni fundi seremala katika eneo la furahisha alisema kuwa kufuatia kuingizwaji wa samani kutoka nnje ya nchi biashara zao zimekuwa zikidorora kutokana na samani hizo huuzwa kwa bei ya chini.

amesema kuwa japo samani hizo uonekana kuwa nzuri kwa mtazamo, na zenye bei nafuu kwa wateja,tayari baadhi ya wateja  wameshabaini kuwa ni hafifu ambapo kwa sasa wameanza kurejea kununua samani zinazotengenezwa hapa nchini.

Bwana Mkumbo ameelezea changamoto  zinazo wakabili  kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji,ukiritimba wa hutoaji mikopo  pamoja  na mali ghafi mbao, ambazo uuzwa kwa bei ya juu,jambo ambalo huwafanya wao  kuuza samani hizo kwa bei ghali ukilinganisha na samani kutoka nje ya nchi.

Kwa upande wao baadhi ya wanunizi wa samani hizo wameeleza tofauti ya bidhaa hizo wakisema kuwa samani za ndani ni imara kuliko za nnje lakini wao ulazimika kutonunua za nje kutoka na bei yake kuwa nafuu ukilinganisha na zile za hapa nchini.

Akizungumzia hilo mkaazi wa eneo la Nyamanoro jiji mwanza bwana Samwel Mayunga amesema kuwa samani za nnje huharibika mapema tofauti na zile zinazotengenezwa hapa nchini ambazo mwananchi wa kawaida hamudu kuzinunua,na kuimba serikale kupunguza gharama ya malighafi mbao, sambamba na ushuru ili mwananchi aweze kununua samani za hapa nchini kama ilivyo kwa zile za nnje.  

Aidha wajasiria mali hao wa samani za hapa nchini wameiomba serikale kuzuia uangizwaji wa samani kutoka nnchi ya nnje ili kujanga mazoea kwa watanzania kununua bidhaa za hapa nnchini na hatimaye kuinua uchumi wa taifa lao.


Sunday, April 29, 2012

AJALI YA COAST LINE

Ajali ya basi la kampuni ya Coast Line linalofanya safari yake kutoka arusaha kupitia Simanjiro,Kitento hadi Dodoma jana katika kijiji cha Terrat wilayani simanjiro mkoani manyaara.baada ya kugoga mti ulioko kando ya barabara

 by Jackson Mollel o.r.s fm

Saturday, April 28, 2012

BASI LA LA COAST LINE LAPATA AJALI MKOANI MANYARA LIKITOKEA ARUSHA KWENDA DODOMA


Na Wilberd Kiwale
Simanjiro-Manyara


Hili ni basi la Coast line ambalo limepata ajali leo Juma mosi asubuhi katika kijiji cha Terrat kilichopo wilayani Sianjiro Mkoani Manyara,likitokea Arusha likielea Dodoma.



Zaidi ya abiria hamsini wamenusurika kufa baada ya basi la kampuni ya Coast line  walilokua wakisafiria kutoka mkoani Arusha kuelekea Mkoani Dodoma   kupasuka tairi  na kugonga mti katika kijiji cha Terrat Wilayani Simanjiro  mkoani Manyara.

Dereva wa gari hilo  aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani Musa  ambaye amevunjika mguu amesema Ajali hiyo imetokea  ghafla baada ya moja ya magurudumu ya mbele ya basi hilo kupasuka wakiwa katika mteremko  hali  iliyomfanya kushindwa kuhimili usukani na kugonga  mti uliokuwa pembeni mwa bara bara hiyo.



           Hawa ni baadhi ya abiria walionusurika katika Ajali hiyo

 

Na huu ndio mti wa Mgunga ambao Basi hili la COAST LIME limeugonga baada ya Kupasuka magurudumu ya mbele.