Imebainika kuwa hali ngumu ya maisha inayowakabili mafundi seremala wa jiji la mwanza inatokana na ungizwaji wa samani kutoka nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya mafundi hao walipozungumzaa na ors fm hili hivi karibuni, katika maeneo yao jijini humo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake bwana Inocent Mkumbo ambaye ni fundi seremala katika eneo la furahisha alisema kuwa kufuatia kuingizwaji wa samani kutoka nnje ya nchi biashara zao zimekuwa zikidorora kutokana na samani hizo huuzwa kwa bei ya chini.
amesema kuwa japo samani hizo uonekana kuwa nzuri kwa mtazamo, na zenye bei nafuu kwa wateja,tayari baadhi ya wateja wameshabaini kuwa ni hafifu ambapo kwa sasa wameanza kurejea kununua samani zinazotengenezwa hapa nchini.
Bwana Mkumbo ameelezea changamoto zinazo wakabili kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji,ukiritimba wa hutoaji mikopo pamoja na mali ghafi mbao, ambazo uuzwa kwa bei ya juu,jambo ambalo huwafanya wao kuuza samani hizo kwa bei ghali ukilinganisha na samani kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wao baadhi ya wanunizi wa samani hizo wameeleza tofauti ya bidhaa hizo wakisema kuwa samani za ndani ni imara kuliko za nnje lakini wao ulazimika kutonunua za nje kutoka na bei yake kuwa nafuu ukilinganisha na zile za hapa nchini.
Akizungumzia hilo mkaazi wa eneo la Nyamanoro jiji mwanza bwana Samwel Mayunga amesema kuwa samani za nnje huharibika mapema tofauti na zile zinazotengenezwa hapa nchini ambazo mwananchi wa kawaida hamudu kuzinunua,na kuimba serikale kupunguza gharama ya malighafi mbao, sambamba na ushuru ili mwananchi aweze kununua samani za hapa nchini kama ilivyo kwa zile za nnje.
Aidha wajasiria mali hao wa samani za hapa nchini wameiomba serikale kuzuia uangizwaji wa samani kutoka nnchi ya nnje ili kujanga mazoea kwa watanzania kununua bidhaa za hapa nnchini na hatimaye kuinua uchumi wa taifa lao.
No comments:
Post a Comment