Thursday, August 9, 2012

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA MANYARA NA MKUU WA WILAYA YA SIMANJIRO KATIKA KIJIJI CHA TERRAT KUHAMASISHA JUU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA MANYARA NA MKUU WA WILAYA YA SIMANJIRO KATIKA UHAMASISHAJI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo kushoto, mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Supuk Nelukendo na kulia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Simanjiro Brown Ole Suya, wakati wa uhamasishaji wa sensa ya wati na makazi katika kijiji cha Terrat.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Terrat waliofika kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo na Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Kanali Cosmas Kayombo (hawapo pichani) kuhusiana na sensa ya watu na makazi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Supuk Nelukendo akiongea na wananchi, juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu wa 8 nchi nzima.
 Mwanyekiti wa CCM vijana kata ya Loiborsoit Lee Shinini akiuliza swali ili apate ufafanuzi juu ya kuhesabiwa kwa mifugo ya wafugaji ambayo ipo nje wilaya ya Simanjiro.
 Mwananchi wa kijiji cha Terrat Godson Nduya naye akiuliza swali ili aweze kupata ufafanuzi juu ya sensa ya watu na makazi.
Mzee wa kifugaji akimuuliza swali mkuu wa Mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo (hayupo pichani) kuhusiana na sensa ya watu na makazi.
 Afisa matangazo ya nje (PA) wa ORS FM Greyson Martin Orongai, akihakikisha kila kila kinachozungumzwa kinasikika kwa ufasaha kwa kutumia microphone na spika ziliwekwa katika uwanja wa mikutano.
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa ORS FM Baraka David Ole Maika aliyeshika microphone akirekodi yale yanayozungumzwa na Afisa Utamaduni wilaya ya Simanjiro Lameck Nanyaro wakati mkuu wa mkoa wa Manyara na Mkuu wa wilaya ya Simanjiro (hawapo pichani) walipofungua mafunzo ya wakufunzi wa sensa ya watu na makazi katika kijiji cha Terrat jana.


Katika ziara yake ya kutembelea wilaya ya Simanjiro na mkoa wa Manyara, Mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo ametoa hamasa kwa jamii ya kifugaji kujitokeza kushiriki katika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika tarehe 26/08/2012 kote nchini.

Pia amewataka kuachana na dhana iliyojengeka miongoni mwa wengi kuwa kuhesabiwa kwa watu au mifugo kunasababisha kifo.

Bwana Elasto Mbwilo ameitaka jamii ya kifugaji kuanza kulima kilimo chenye tija ili waweze kujihifadhia mazao kwa ajili ya chakula cha baadaye cha familia kuliko kubweteka na kusubiria chakula cha msaada, na ametilia mkazo kuwa mbali na mahindi pia wahakikishe wanapanda mazao yanayostahamili ukame kama vile Mtama na yeye yupo tayari kuwatafutia soko endapo kama watakosa pa kuuzia.


Imerushwa na: Khadija Abdallah
Picha kwa hisani ya Greyson Martin Orongai na Baraka David Ole Maika

No comments:

Post a Comment