Friday, March 30, 2012

Na Julius Laizer
waraka kwa asasi wilayani Kiteto

KITETO

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara,Frank Uhahula amesema atazichukulia hatua kali asasi zisizo za kiserikali ambazo zimeacha kufanya kile walichosajiliwa nacho na kushiriki kuleta uchochezi wilayani humo.

Uhahula ameyasema hayo hivi karibuni mjini Kibaya na kudai kuwa asasi nyingi wilayani humo zimeshiriki kuleta maendeleo ndani ya jamii lakini nyingine zimejivika mwamvuli wa vyama vya kisiasa na kujiingiza kwa kificho kwenye shughuli za kisiasa.

Amesema kuwa asasi hizo badala ya kuendeleza masuala waliyosajiliwa nayo ya maendeleo ndani ya jamii hushirikiana na baadhi ya vyama vya kisiasa katika kufanya uchochezi kwa wananchi.
Bwana huhaula amezitaka asasi hizo kuchague moja, kati ya uanasiasa au uwana harakati wa maendeleo ya kijamii ili watambue kwmba wanashindana nao kama vyama vingine katika kutaka kukamata dola maana hawaeleweki kama ni asasi ama vyama vya kisiasa

Ameongeza kuwa asasi hizo zisimchonganishe Rais Jakaya Kikwete na wananchi wake kwani zinatakiwa kuleta maendeleo kwa wananchi badala ya kujiingiza kisirisiri kwenye mambo ya kisiasa na kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa wilayani humo.

Na Julius Laizer
Uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki

ARUMERU

Chama cha D emokrasia na Maendeleo Chandema kimelitaka jeshi la Polisi kuwa sehemu ya matumaini na haki kwa wana wanchi wa Arumeru Mashariki na sio kuwatisha na kuwatio hofu.
Hayo  yamesemwa na mwenyekitu wa chama cha Demokrasia na Maendelo Chadema mheshimiwa Freman Mbowe katika mikutano aliyoifanya katika jimbo la Arumeru Mashariki, katika vijiji vya Maruango Uwilo,Ushiri,Ambureni na Embaseni ya kumnadi mgombea ubunge wake bwana Joshua Nasari.

Nae manager wa Kampeni wa Chadema Mheshimiwa Vecent Nyerere akizungumza katika mikutano hiyo ameeleza kusikitishwa na kauli ya Chama cha Mapinduzi ya kuwataka wanachama wake kutohudhuria mikutano ya Chadema akisema kuwa ni kuwanyima haki yao ya msingi huku akiwataka wanachama wa Chadema na wapenda maendele kuhudhuria Mikutano ya ccm kusikiliza sera zao.

Kwa upande wake chama cha Mapinduzi kimeitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuchukua hatua za kisheria kwa wanachama na viongozi wa vyama vya Upinzani wanaomdhalilisha mgombea wa chama hicho bwana Sioi Sumari kwa kuzichana,ama kusipaka wanja na kuchora herein masikioni katika picha za mgombea huyo na kisha kuzibadika mitaani

Mratibu wa kampeni za chama hicho na mbunge wa Simanjiro Mheshimiwa Christofa ole Sendeka amesema vitendo hivyo vinaweza kusababisha machafuko endapo wafuasi wa chama kinocho tendewa hayo wakiamua kujibu mapigo kwa kuwa wanaofanya hivyo wanafahamika.

Monday, March 26, 2012

BWILO AKAMILISHA ZIARA SIMANJIRO

NADONJUKIN  SIMANJIRO


Na Jackson Mollel

Ziara ya Siku nne ya Mkuu wa mkoa wa manyara Bwana Elaston John Bwilo wilayani Simanjiro mkoani Manyara imekamilika katika kijiji Cha Nadonjukin kwa yeye kupokea kero na malalamiko mbalimali ya wakazi wa kijiji hicho.

Katika kikao hicho kilichokuwa na idadi kubwa ya kina mama  wa jamii ya Kimaasai wakazi wa kijiji hicho ambapo baathi yao walifika ofisini kwa mkuu wa Mkoa mjini Babat walisema kuwa sambamba na mambo mengine yaliyo kero  katika kijiji hicho, kubwa ni Uwekezaji wa Kampuni ya Ranchi ya Ormoti Tukuta Conservation  waliopo katika eneo lao.

Wamama hao waliwasilisha kero zao kwa mkuu huyo kwa kusoma risala iliyojaa tuhuma kwa kampuni ya Ormoti Tukuta Conservation ya kuwa wamepewa eneo lililo katika kijiji chao bila ya ridhaa yao.

Mara baada ya Risala hiyo iliyosomwa na  bibi Naomi Mbatiany,  Mkuu wa Mkoa  bwana Bwilo amesema kuwa kuna haja ya Kuchunguza jambo hilo kwa kina katika kufuata taratibu za kisheria ili kuweza kulipatia Ufumbuzi mapema. 
 
Bwana Bwilo amesema kuwa si rahisi kwa yeye kutamka mara moja ya kuwa eneo ni la nani lakini ameahidi kutuma wataalam wa ardhi kutoka mkoa ili kuja kubaini mipaka jambo litakaloleta Suluhu katika mgogoro huo.

Katika Kikao Hicho  kilicho Hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikale kutoka Mkoa na Wilaya, Mbuge wa Simanjiro mheshimiwa Christopha ole Sendeka alimuomba mkuu wa Mkoa kushirikisha wazee na viongozi wa Zamani katika zoezi hilo la kubaini mipaka hiyo.

Ole Sendeka amesema kuwa taratibu na mipango ya utoaji wa Ranchi hiyo haukufuata taratibu zinazo Stahili huku akimwomba mkuu huyo kuunda Tume itakayo chunguza nyaraka mbalimbali za uhalali wa kuwepo kwake katika eneo hilo.
                    

SUKURO SIMANJIRO. ENG`ENO WAPATA NYUMBA YA WAALIMU.


SUKURO SIMANJIRO 

 Na Jackson Mollel

Waananchi wa kijiji cha Sukuro wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wametakiwa kujiwekeza katika Elimu na ufgaj, ili kujiletea maendeleo endelevu katika Nyanja ya Kiuchumi
Hayo yameelezwa na  mkuu wa Mkuu wa mkoa wa Manya

 Bwana Elaston John Bwilo wakati akifungua na kuweka jiwwe la Msingi katika nyumba ya watumishi wa shule ya sekoondari ya Kata ya Komolo Eng`eno iliyopo katika kijij Cha Sukuro  Wilayani Simani mkoani  Manyarai

Katika ziara yake shuleni hapo Mkuu alielezwa changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na tatio la maji uchache wa walimu ukosefu wa chakula kwa wanafunzi sambamba na upukfu wa samani mbalimbali kwa walimu na wanafunzi.


Wakati akitoa hotuba yake  kwa wakazi wa kijiji hicho waliohudhuria ufunguzi huo, aliwataka kutoa Idadi kamili ya Mifugo yao ili  kuweza kuweka mipango halis ya matibabu,ujenzi wa majosho,Banio pamoja na miundo mbinu mingine kwa lengo la kuboresha afya ya mifugo wilayani humo kama taaluma ya mifugo inavyo elekeza.

Katika taarifa iliyotolewa Shuleni hapo kuhusu  watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Kwanzi mwaka huu  wa 2012 ambao hawakuripoti shuleni hapo mkuu huyo alitoa agizo kumwagiza mkuu wa Wilaya ya Simanjiro bwana Khalidy Mandiya kufuatilia na kuwakamata wazazi wote waliogairi kuwapeleka watoto shuleni.

Sunday, March 25, 2012



LOON`DEREKES SIMANJIRO

Mkuu wa mkoa wa Manyara bwana  Elaston John Bwilo amezindua Mradi wa Maji katika kijijicha Londerkes kata ya Kitwai Wilayani Simanjiro mkoani Manyara Uliogharimu jumla ya shilingi Milioni 59 laki tisa 9 na 42 elfu

Kijiji hicho ambacho ni kati ya vijiji 52 vya wilaya ya Simanjiro ni miongoni mwa vijiji vilivyo na tatizo la uhaba wa maji ambapo wakazi wake wanalazimika kuchota maji katika chemchem iliyopo umbali mrefu kutoka kijijini hapo.

Habari kutoka Loondrekes zinasema kuwa awali wakaza wa kijiji hicho walikuwa wanapaata maji katika Chemchem iliyopo mlimani, ambapo wanawake na watoto wakazi wa kijiji hicho wemekuwa wakipata tabu wakati wa kwenda kuteka maji kutokana na muinuko mkali wa mlima huo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mkuu huyo ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kupitia Vikao vya madiwani kuangalia kwa zaidi kwa macho mawili suala la mifugo kwani ndiyo uchumi pekee unaotengemewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa wilaya ya Simanjiro.

Bwana Bwilo ameiomba Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Kupitia Idara ya Mifugo kujenge Majosho ya kisasa kwaajili ya kuogesha mifugo pamoja na kupatiwa Chanjo  na mahitaji mengine muhimu kwa kadri taaluma ya mifugo inavyoelekeza. 

               By Jackson M Mollel (KIONGOZI)

Saturday, March 24, 2012

MIUNDO MBINU WILAYANI SIMANJIRO BADO NI KIKWAZO CHA MAENDELEO
                                     Hii ni sehemu ya daraja lililoharibiwa na mvua na kusababisha
                                     adha kwa wananchi na wasfiri ndani ya wilaya ya Simanjiro na
                                     wilaya ya Kiteto

TERRAT-SIMANJIRO 24/3/2012
Na Julius Laizer
Wananchi wa kijiji cha Terrat na maeneo mengine wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wameiomba serikali kuhakikisha kuwa inarekebisha miundo mbinu ya bara bara ili kuwarahisishia majukumu yao mengi hasa kipindi hiki cha mvua

Wameyasema hayo kutokana na daraja lililoharibika katika kijiji cha Komolo na kuwasababishia ugumu wa usafiri wa wananchi watokao mji wa Arusha kuelekea makao makuu ya Wilaya na wanaoelekea Wilayani Kiteto

Daraja hilo limehaibika kufuatia mvua zilizonyesha mwaka jana na kubomoa sehemu kubwa ya daraja hilo hali iliyosababisha magari na wananchi kushindwa kulitumia na badala yake wanapita kwa pembeni

Jamii imeomba serikali kuchukua hatua za haraka kukarabati daraja hilo kwa kiwango cha hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wananchi wa wanafunzi wanapata usafiri kwa muda na wakati unaostahili

Wakielezea adha ya daraja hilo wafanyabiashara na waendesha magari wamesema mvua inaponyesha korongo hilo kupitisha maji mengi ambapo huwafanya wasubiri mpaka maji yapungue ndipo wapite hivyo bidhaa wanazobeba hurabika na kufika vikiwa vimepungua ubora wake hasa zile za sokoni

Friday, March 23, 2012

MRADI WA MAJI WAZINDULIWA LOON`DERKES



LOON`DEREKES SIMANJIRO

Mkuu wa mkoa wa Manyara bwana  Elaston John Bwilo amezindua Mradi wa Maji katika kijijicha Londerkes kata ya Kitwai Wilayani Simanjiro mkoani Manyara Uliogharimu jumla ya shilingi Milioni 59 laki tisa 9 na 42 elfu

Kijiji hicho ambacho ni kati ya vijiji 52 vya wilaya ya Simanjiro ni miongoni mwa vijiji vilivyo na tatizo la uhaba wa maji ambapo wakazi wake wanalazimika kuchota maji katika chemchem iliyopo umbali mrefu kutoka kijijini hapo.

Habari kutoka Loondrekes zinasema kuwa awali wakaza wa kijiji hicho walikuwa wanapaata maji katika Chemchem iliyopo mlimani, ambapo wanawake na watoto wakazi wa kijiji hicho wemekuwa wakipata tabu wakati wa kwenda kuteka maji kutokana na muinuko mkali wa mlima huo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mkuu huyo ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kupitia Vikao vya madiwani kuangalia kwa zaidi kwa macho mawili suala la mifugo kwani ndiyo uchumi pekee unaotengemewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa wilaya ya Simanjiro.

Bwana Bwilo ameiomba Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Kupitia Idara ya Mifugo kujenge Majosho ya kisasa kwaajili ya kuogesha mifugo pamoja na kupatiwa Chanjo  na mahitaji mengine muhimu kwa kadri taaluma ya mifugo inavyoelekeza. 

               By Jackson M Mollel (KIONGOZI)

Friday, March 16, 2012

HANANG

WAZAZI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO.

Hanang-Manyara

Na Wilberd Kiwale
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani manyara Winfrida Ligubi,amewataka wakazi wa kata ya Balangdalalu kutoa ushirikiano wa ulinzi wa shule ya secondary ya Bweni ya Balangdalalu,dhidi ya matukio ya kuungua moto.


Kanali Mstaafu Ligubi ametoa agizo hilo,kutokana na matukio ya kuzuka moto mara Kwa mara kwenye Shule hiyo,na kusababisha kufungwa kwa kipindi cha mwezi Mmoja Kwa ajili ya kukarabatiwa.

Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo juzi kwenye kikao cha Bodi ya Shule hiyo,alipoitembelea kuona Maendeleo ya ukarabati wa Bweni Moja na madarasa mawili yaliyoungua moto kwa siku tofauti. 


Matukio ya kuungua moto kwa mabweni yalitokea Januari 31 Mwaka Huu na tukio la pili kuungua moto Kwa madarasa mawili yalitokea  Februari 16 Mwaka Huu na Chanzo cha kuzuka moto huo kikiwa bado hakijabainika.

Mkuu wa Shule hiyo GodlivingTyaso amesema ukarabati wa mabweni na madarasa mwili yaliyoungua unaendelea vizuri,ingawa hawakupata Msaada wowote zaidi ya Mfuko wa maafa,na amesema wanafunzi wanatarajia kurudi shuleni mwezi huu wa tatu tarehe 18.
MCHIMBAJI WA MADINI AKUTWA AMEFARIKI...


SIMANJIRO-MANYARA


Na Wilberd Kiwale
Mchimbaji mdogo wa Madini ya Tanzanite (MwanaApolo) wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,amekutwa amefariki Dunia pembeni ya barabara kwenye machimbo ya Madini Hayo.

Kamanda wa polisi Mkoani Manyara Kamishna msaidizi Liberatus Sabas,amemtaja marehemu kuwa nai Jimmy Chawe (25) mkazi wa kitongoji cha Songambele,katika Mji mdogo wa Mirerani.

Kamanda Sabas amesema Chawe amekutwa amekufa siku ya jumatatu saa 12:30 asubuhi,kwenye barabara iliyopo kwenye machimbo ya Madini ya Tanzanite eneo la Mpaka wa kitalu D na kitalu C Mji mdogo wa Mirerani.

Chanzo cha kifo cha mchimbaji huyo ambaye ana Asili ya Kijiji cha Pomelini Mkoani Iringa hakijafahamika mara Moja,na alikutwa akiwa na jeraha dogo kwenye mguu wa kushoto.

Kamanda Sabas alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha (Mount Meru) Kwa ajili ya uchunguzi zaidi Kabla ya kusafirishwa kupelekwa Mkoani Iringa.