Monday, July 9, 2012

ILIVYOKUWA AJALI YA COAST LINE

by Jackson Mollel.                     MAKALA KATIKA PICHA


AJALI YA BASI LA KAMPUNI YA COAST LINE 28/04/2012  HASUBUHI LINALOFANYA SAFARI KATI YA ARUSHA NA DODOMA KUPITIA WILAYA ZA SIMANJIRO NA KITERO









SHINA LA MGUGA ULIYOGONGWA NA BASI
ENEO LA AJALI KATIKA KIJIJI CHA TERRAT WILAYANI SIMANJIRO MKOANI MANYARA


KUSHOTO NI DREVA WA BASI HILO BWANA RAMADHANI ALIYEVUNJIKA MGUU WA KULIA NA MWINGINE KUPATA MAJERAHA MAKUBWA
MTOTO ALIYERUSHWA KUPITIA KIOO  CHA MBELE NA AKATOKA SALAMA BILA HATA JERHA LOLOTE


ABIRIAALIYEJULIKANA KWA JINA LO LOHANGA ALIPANWA KIFUA NA KUPATA MAJERAHA KICHWANI




WAUGUZI KATIKA ZAHANATI YA TERRAT WAKITOA HUDUMA YA KWANZA KWA MAJERUHI
BAADA YA HUDUMA YA KWANZA SAFARI ILIANZA KUELEKEA KIJIJI JIRANI CHA LOSWAKI KILIPO KIWANJA CHA NDEGE CHA FLYING MADICAL SERVICE KM SABAKUTOKA ILIPO ZAHANATI YA TERRAT MAJERUI WAPELEKWE  MJINI ARUSHA


MAJERUHI WAKIWA KWENYE  GARI LA TAASISI YA ILARAMATAK LORKONEREI LILILOWAPELEKA UWANJA MDOGO WA NDEGE KIJIJINI LOSWAKI

NDEGE YA FLYING MEDICAL SERVICE KATIKA KIJIJI CHA KOSWAKI DAKIKA KUMI NA SITA TANGU IMEITWA KUTOKA UWANJA WA NDEGE KISONGO MJINI ARUSHATAWARI KWA KUWAPELEKA MAJERUHI.



 
MAJERUHI LOHANGA AKIPATIWA HUDUMA NA PADRI RUBANI WA NDEGE YA FLYING MEDICAL SERVICE KABLA YA KUPAKIWA KWENYE NDEGE .
LUHANGA AKUPAKIWA KWENYE NDEGE KWA MSAADA WA WAKAZI WA KIJIJI CHA TERRAT NA OLOSWAKI MAJIRA YA SAA NANE MCHANA





                        

NA NDEGE IKAWA TAYARI KUONDOKA IKIWA MAJERUHI WOTE WAMEPAKIWA  KUELEKEA UWANJA MDOGO WA NDEGE KISONGO MKOANI ARUSHA


 

NA BAADAE TUKAREJEA TENA KATIKA ENEO LA TUKIO  




 

HUYU NI BABA WA MTOTO WA ALIYENUSURIKA AKIWA NA MWANAE











MAFUNDI SEREMALA MWANZA WALALAMIKIA HALI NGUMU YA MAISHA

Jackson Mollel

Imebainika kuwa hali ngumu ya maisha inayowakabili mafundi seremala wa jiji la mwanza inatokana na ungizwaji wa samani kutoka nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya mafundi hao walipozungumzaa na ors fm hili hivi karibuni, katika maeneo yao jijini humo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake bwana Inocent Mkumbo ambaye ni fundi seremala katika eneo la furahisha alisema kuwa kufuatia kuingizwaji wa samani kutoka nnje ya nchi biashara zao zimekuwa zikidorora kutokana na samani hizo huuzwa kwa bei ya chini.

amesema kuwa japo samani hizo uonekana kuwa nzuri kwa mtazamo, na zenye bei nafuu kwa wateja,tayari baadhi ya wateja  wameshabaini kuwa ni hafifu ambapo kwa sasa wameanza kurejea kununua samani zinazotengenezwa hapa nchini.

Bwana Mkumbo ameelezea changamoto  zinazo wakabili  kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji,ukiritimba wa hutoaji mikopo  pamoja  na mali ghafi mbao, ambazo uuzwa kwa bei ya juu,jambo ambalo huwafanya wao  kuuza samani hizo kwa bei ghali ukilinganisha na samani kutoka nje ya nchi.

Kwa upande wao baadhi ya wanunizi wa samani hizo wameeleza tofauti ya bidhaa hizo wakisema kuwa samani za ndani ni imara kuliko za nnje lakini wao ulazimika kutonunua za nje kutoka na bei yake kuwa nafuu ukilinganisha na zile za hapa nchini.

Akizungumzia hilo mkaazi wa eneo la Nyamanoro jiji mwanza bwana Samwel Mayunga amesema kuwa samani za nnje huharibika mapema tofauti na zile zinazotengenezwa hapa nchini ambazo mwananchi wa kawaida hamudu kuzinunua,na kuimba serikale kupunguza gharama ya malighafi mbao, sambamba na ushuru ili mwananchi aweze kununua samani za hapa nchini kama ilivyo kwa zile za nnje.  

Aidha wajasiria mali hao wa samani za hapa nchini wameiomba serikale kuzuia uangizwaji wa samani kutoka nnchi ya nnje ili kujanga mazoea kwa watanzania kununua bidhaa za hapa nnchini na hatimaye kuinua uchumi wa taifa lao.